Joy FM

Madereva wanaopaki maroli pembezoni mwa barabara kushushiwa rungu

4 February 2025, 10:53

Mwenyekiti wa halmashauri ya Mji Kasulu Bw. Noel Hanula, Picha na Emmanuel Kamangu

Madereva wa maroli katika Halmashauri ya Mji wa Kasulu wametakiwa kuzingatia sheria na kuacha kupaki magari yao pembezoni mwa barabara.

Na Emmanuel Kamangu

Baraza la madiwani  halamshauri ya mji wa Kasulu limemuagiza mkurugenzi wa mji kasulu kuhakikisha anawashugulikia madereva wote wa maroli yanayopaki kiholea barabarani.

Uamzi huo umekuja Kufuatia hoja ambayo imeibuliwa na diwani wa kata ya mrumbona Bw, Emmanuel Kisunzu katika kikao cha Baraza la madiwani cha robo ya pili ya mwaka  2024-2025  ambapo    imemlazimu mwenyekiti wa baraza hilo Bw, Noel Hanula kutoa maelekezo kwa mkurugenzi ili kuhakikisha madereva wote wa magari makubwa wanaopaki kiholela katika mji wa kasulu kuchukuliwa hatua ikiwemo kutozwa faini.

Wakuu wa idara mbalimbali Halmashauri ya Mji wa Kasulu wakiwa katika kikao cha madiwani, Picha na Emmanuel Kamangu

Aidha Bw.  Hanula amesema maroli yote yanatakiwa kupaki maeneo maalumu yaliyotengwa ya stendi mpya ili kuepuka kupaki kiholela pembezoni mwa barabara za mji wa kasulu jambo linaweza kusababisha ajali na kuondoa usalama kwa wananchi.

Kwa upande wake, Kaimu mkurugenzi halmashauri ya mji wa kasulu Bw, Joseph Jumbe amesema wamejipanga kukabiliana na kero hiyo ili madreva wote wa maroli wanaopaki  pembezoni mwa barabara waweze kuchukuliwa hatua za kisheria.

Kaimu mkurugenzi halmashauri ya mji wa kasulu Bw, Joseph Jumbe, Picha na Emmanuel Kamangu

Hata hivyo diwani wa kata ya mrusi ambapo ndiko kuna stend maalumu kwa ajili ya maroli  Bw, Fanuel kisabo amesisitiza swala hilo la magari kupaki kiholela lishugulikiwe kwa wakati ili kuondokana na kero hiyo.

Ripoti ya mwanahabari wet Emmanuel Kamangu