

31 January 2025, 13:07
Watumishi wa umma Wilayani Buhigwe Mkoani Kigoma wametakiwa kufanya kazi kwa kuzingatia utawala bora ili kuhakikisha wanafikia azma ya kufikisha maendeleo kwa wananchi.
Na Emmanuel Kamangu
Katibu tawala wa Wilaya ya Buhigwe Utefta Mahega amewataka Watumishi wa umma Wilaya ya Buhigwe kuzingatia Demokrasia na Utawala bora ili kuendelea kujenga imani kwa Wananchi dhidi ya Serikali yao ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Bi Mahega amesema hayo katika mafunzo ya Elimu ya Uraia na Utawala bora ambayo yameandaliwa na Wizara ya Katiba na Sheria Kwa watalamu mbali mbali katika Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe yakilenga kutoa ufahami katika kuhakikisha wanasimaia haki na sawa katika jamii.
Aidha Bi Joyce Mushi ambaye ni Wakili wa Serikali kutoka Wizara ya Katiba na Sheria na Mratibu wa mafunzo hayo amesema lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo viongozi wa Serikali za Mitaa ili kutatua changamoto na malalamiko katika jamii kwa kuzingatia demokrasia.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe NGeorge Emmanuel Mbilinyi ameishukuru Wizara ya Katiba na Sheria kwa kuleta mafunzo hayo na kuwasihi watumishi hao kutumia mafunzo hayo katika utendaji wao wa kazi.
Hata hivyo baadhi ya watenji wa kata na vijiji ambao wameshiriki mafunzo hayo wamesema yatawasaidia Kwa kiasi mkubwa kuendelea kusimamia haki na utawala bora katika jamii.