

31 January 2025, 11:25
Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) mkoa wa Kigoma imebaini mapungufu madogo madogo katika miradi 31 ya maendeleo kati ya miradi 32.
Na Orida Sayon
Akitoa taarifa ya ufuatiliaji wa miradi ya maendeleo katika kipindi cha kuanzia mwezi wa oktoba hadi Disemba 2024, Naibu Mkuu wa Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa kigoma John Mgallah amesema kuwa taasisis hiyo imefuatilia utekelezaji wa miradi ya maendeleo 32 yenye thamani ya Tsh. 11,453,699,642.67/=
Sauti ya Naibu mkuu TAKUKURU
Mgallah amesema miongoni mwa miradi yenye mapungufu ni katika ujenzi bweni 1, madarasa 3 na matundu 6 ya vyoo katika shule ya Sekondari Nyarubanda yenye thamani ya Mil.341,600,000/= kama anavyoeleza
Baadhi ya wananchi mkoani Kigoma wametoa maoni yao juu ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo na kwamba imekua ikicheleweshwa kukamilika kwa wakati huku mingine ikikamilika haipo kwenye ubora wake na kuomba serikali kuchukulia hatua wote wanaohusika na ucheleweshwaji wa miradi hiyo.
Kuzuia rushwa ni jukumu lako na langu ;tutimize wajibu