

28 January 2025, 14:37
Serikali imesema itahakikisha inawafikia watoto katika zoezi la usambazaji wa chanzo katika wilaya za mkoa wa kigoma
Na Josephine Kiravu
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Thobias Andengenye amekabidhi pikipiki 12 pamoja na gari moja kwa ajili ya kusambaza chanjo katika maeneo mbalimbali mkoani Kigoma na kuwataka watumishi kuvitumia vizuri vyombo hivyo ili walengwa wote wa chanjo wapatiwe kwa wakati.
Awali akizungumza katika hafla hiyo, Mganga mkuu Mkoa wa Kigoma Dr Damas Kayera amesema hali ya utoaji chanjo Kwa mkoa wa Kigoma ni nzuri na kwamba vifaa hivyo vitasaidia kuongeza idadi ya watoto watakaopatiwa chanjo Kwa kufika maeneo yote ya mkoa.
Na hapa mkuu wa mkoa wa Kigoma ambae alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo amesisitiza uadilifu na kujituma kazini Kwa watumishi.
Kwa upande wake, Mkuu wa wilaya ya Kigoma Dr Rashid Chuachua kwa niaba ya wakuu wakuu wa wilaya zingine ameahidi kutumia vyombo hivyo kwa kazi iliyokusudiwa.