Waziri Mbarawa aitaka TPA Kigoma kuimarisha utendaji kazi
24 January 2025, 09:06
Serikali imesema kuwa itaendelea kuboresha bandari nchi kwa lengo la kuwavutia wawekezaji kutoka ndani na nje ya nchi.
Na Kadislaus Ezekiel
Waziri wa Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa amesema Serikali imedhamiria kuufungua mkoa wa kigoma kupitia sekta ya usafirishaji kwa njia ya maji kwa kuboresha miundombinu ya bandari za ziwa Tanganyika zinaendelea Hatua itakayo chagiza mzunguko mkubwa kibiashara na Nchi Jirani za CONGO DRC NA BURUNDI, na kukuza Uchumi kwa kasi.
Akikagua Miundombinu ya Bandari ya Kigoma Waziri Mbarawa, amebainisha kuwa, ukarabati wa Bandari za Ziwa Tanganyika na ujenzi wa Meli za mizigo na abiria ni chachu ya kukuza uchumi na kuvutia wawekezaji Nchini hasa ukanda wa Maziwa Makuu.
Meneja wa Bandari za Ziwa Tanganyika Edward Mabula, amesema Bandari ya Kigoma ni Kitovu cha Biashara Katika kusafirisha Mizigo inayoenda nchi jirani ya Congo DRC, Huku Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania Juma Kijavara akieleza kuwa, ujezni wa Reri ya Kisasa na Meli za Mizigo na abiria ni muhimu katika kukuza uchumi kupitia sekta ya usafirishaji.