Joy FM
Wakuu wa kaya watakiwa kujenga vyoo bora
20 January 2025, 11:44
Ujenzi wa vyoo bora kwa kila kaya inatajwa kuwa sehemu ya mapambano dhidi ya magonjwa ya mlipuko ikiwemo kipindupindu.
Na Michael Mpunije
Wakuu wa kaya Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu Mkoani Kigoma wametakiwa kujenga vyoo bora na kuzingatia kanuni za unawaji mikono ili kukabiliana na magonjwa ya mlipuko.