Joy FM

Watoto waliofaulu wapelekwe kidato cha kwanza

20 January 2025, 11:06

Mkuu wa wilaya ya Kasulu Kanali Isack Mwakisu ,-picha na Hagai Ruyagila

Kila mzazi ana wajibu wa kuhakikisha mtoto wake anapata haki ya elimu bora na elimu bora huanza na maandalizi bora kwa mtoto.

Na Hagai Ruyagila

Wazazi na walezi wilayani Kasulu mkoani Kigoma wametakiwa kutambua umuhimu wa elimu kwa kuwapeleka shule watoto wao waliofaulu kujiunga elimu ya sekondari pamoja na darasa la awali na msingi ili wawezi kutimiza ndoto zao.

Rai hiyo imetolewa na mkuu wa wilaya ya Kasulu Mkoani Kigoma Kanali Isaac Mwakisu wakati akizungumza na wazazi pamoja na baadhi ya viongozi wa serikali za vijiji halmshauri ya wilaya ya Kasulu.

Kanali Mwakisu amesema atawachukulia hatua za kisheria wazazi watakaoshindwa kuwapeleka shule watoto wao kwani kitendo hicho ni kumyima haki za msingi mtoto kupata Elimu na kwamba serikali inaendelea kuboresha miundombinu ya elimu ili kuhakikisha wanafunzi wanasoma katika mazingira mazuri.

Sauti ya Mkuu wa wilaya Kasulu Kanali Isack Mwakisu

Aidha Kanali Mwakisu ameongeza kwa kuwataka wakuu wa shule kuhakikisha wanawapokea watoto wote ambao  hawana sare za shule waweze kuendelea na masomo wakati  wazazi wakiendelea kutafuta  sare hizo.

Sauti ya Mkuu wa wilaya ya Kasulu

Baadhi ya wazazi na walezi Wilayani  Kasulu akiwemo Josephine Shemu na Silivanus Buhengeli wamesema ni muhimu jamii kutambua umuhimu wa Elimu kwa kuhakikisha watoto wanaandikishwa kuanza darasa la awali na msingi pamoja na wale waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza.

Sauti za wazazi na walezi