Wavuvi washauriwa kufuga samaki kutumia vizimba
8 January 2025, 13:05
Ili kuhakikisha samaki zinaongezeka ndani ya ziwa Tanganyika, serikaliimeendelea kuweka mikakati mbalimbali ya kuwawezesha wavuvi na kuwahimiza kutumia vizimba ambavyo vitatumika kwa ajili ya ufugaji wa samaki na kusaidia kuharibu mazalia ya samaki ndani ya ziwa hilo.
Na Timotheo Leonard – Kigoma
Wafugaji na Wavuvi wa Samaki Mkoani Kigoma wameshauriwa kujikita kwenye Uvuvi wa Samaki kwa njia ya vizimba kwani unasaidia kupunguza idadi ya wavuvi ziwani na kuongezeka kwa mazalia ya samaki ziwani.
Uvuvi Nchini Tanzania ni mojawapo ya sekta za uchumi ambayo huchangia ukuaji wa uchumi wa Tanzania kwa kuuza samaki ndani nan je ya nchi hivyo husaidia serikali kupata fedha za kigeni.
Licha ya sekta hii kuchangia ukuaji wa uchumi bado wavuvi na wafugaji wanahimizwa kufuga kisasa kama anavyoeleza Afisa mfawidhi Ziwa Tanganyika kanda ya Magharibi Bw. Agnely Adrian Lishela.
Hata hivyo Bw. Lishela amewataka Wavuvi kukata Leseni za Uvuvi na biashara katika kipindi hiki ambacho zoezi linaendelea, kwani kushindwa kufanya hivyo ni kwenda kinyume na sheria za uvuvi.