Vijana waomba kupewa elimu ya Kujitegemea Kigoma
11 December 2024, 16:12
Ili kuwa na vionozi wenye maadili mema vijana wanapaswa kuandaliwa wakiwa bado katika umri mdogo
Na Josephine Kiravu
Baadhi ya vijana Mkoani Kigoma wameiomba Serikali kuwapatia elimu ya kujitegemea ili kuondokana na dhana ambayo imejengeka kwamba vijana wengi wamekuwa wapambe wa watu hivyo kukosa sifa za kuwa viongozi bora wa baadae.
Vijana hao akiwemo Ayubu Chacha na Brightness Manase wameeleza hayo mara baada ya kumalizika kwa madahalo uliowakutanisha wanafunzi wa TIA na maofisa kutoka TAKUKURU na Sekretarieti ya maadili kutoka kanda ya magharibi ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya maadili.
Sauti za baadhi ya Vijana.
Kwa upande wake, Ofisa kutoka Sekretarieti ya maadili ya viongozi kutoka ofisi ya kanda ya magharibi Tabora Vupala Mbwilo amesema wameamua kufanya mdahalo na wanafunzi ili kuwajengea uwezo kwenye uongozi na kuwafanya wapate hamasa ya kushiriki kwenye uchaguzi na kuchagua viongozi waadilifu.
Sauti ya Ofisa kutoka Sekretarieti ya maadili ya viongozi kutoka ofisi ya kanda ya magharibi Tabora Vupala Mbwilo
Na hapa anaeleza hali ya maaadili kwa viongozi huku akiwataka wale ambao wanaenda kinyume kurekebisha mienendo yao kwa maslahi ya taifa.
Sauti ya Ofisa kutoka Sekretarieti ya maadili ya viongozi kutoka ofisi ya kanda ya magharibi Tabora Vupala Mbwilo
Kauli mbiu ya maadhimisho hayo ya siku ya maadili na haki za binadamu kwa mwaka 2024 ni Tumia haki yako ya Kidemokrasia chagua viongozi waadilifu na wanaozingatia haki za binadamu na misingi ya utawala bora kwa maendeleo ya Taifa.