Joy FM
Watumishi 7 kukatwa asilimia 15 ya mshahara wao Kibondo
19 November 2024, 10:34
Baraza la madiwani la halmashauri ya Wilaya ya Kibondo limeadhimia watumishi Saba wa idara ya afya kukatwa asilimia 15 ya mshahara wao kwa kipindi cha miaka mitatu na kurudisha fedha zaidi ya milioni 70 walizohujumu Serikali kwa kuuza dawa na vifaa tiba kinyume na utaratibu.