Joy FM

Watoto 5,632 kuandikishwa na 2001 kurejeshwa kwa kukatisha masomo Kigoma

12 November 2024, 11:10

Kampeni ya kuwaandikisha na kuwarejesha shuleni watoto walio nje ya mfumo wa shule ngazi ya elimu ya msingi imezinduliwa mkoani kigoma ikiwa na lengo la kukabiliana na changamoto zinazosababisha wanafunzi wanafunzi kutoandikishwa kuanza shule au kukatisha masomo yao.

Na Josephine Kiravu – Kigoma

Mkoa wa Kigoma umejipanga kuandikisha watoto 5,632 na kurejesha watoto 2001ambao walikatisha masomo kutokana na changamoto mbalimbali ikiwemo migogoro ya kifamilia pamoja na imani za kishirikina.

Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Kamishna Jenerali mstaafu wa Jeshi la zimamoto na uokoaji Thobias Andengenye ameeleza hayo wakati akitoa tathmini kuhusu hali ya elimu kwa watoto kuanzia umri wa miaka 7-15 ambapo amesema kwa mwaka 2024 pekee watoto wapatao 7,475 wapo nje ya mfumo wa shule.

Sauti ya Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Kamishna Jenerali mstaafu wa Jeshi la zimamoto na uokoaji Thobias Andengenye
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Kamishna Jenerali mstaafu wa Jeshi la zimamoto na uokoaji Thobias Andengenye akiwa katika kikao na wadau wa elimu, Picha na Josephine Kiravu

Amesema kulingana na utafiti uliofanyika watoto wengi wameshindwa kuendelea na masomo kutokana na vikwazo kadhaa ikiwemo wazazi kuwatumia watoto kwenye kazi za shambani, imani za kishirikina pamoja na adhabu ambazo zimekuwa zikitolewa shuleni.

Sauti ya Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Kamishna Jenerali mstaafu wa Jeshi la zimamoto na uokoaji Thobias Andengenye

Kwa upande wake, Afisa elimu kutoka shirika la kuhudumia watoto duniani UNICEF, Farida Sebalua amesema malengo ya kampeni hiyo ni kurejesha watoto laki moja kwa mikoa ya Kigoma, Tabora na Songwe kwa kipindi cha miaka 5.

Sauti ya Afisa elimu kutoka shirika la kuhudumia watoto duniani UNICEF, Farida Sebalua

Bi Christina Mayaba ni mama ambaye anaishi na binti yake wa kidato cha kwanza, na binti huyo ametoroka kutoka nyumbani baada ya mzazi wake kumhimiza kuzingatia elimu kama anavyoeleza.

Sauti ya Bi Christina Mayaba ni mama ambaye anaishi na binti yake wa kidato cha kwanza

Kampeni hii ya uandikishaji na urejeshaji shuleni watoto walio nje ya mfumo rasmi wa shule inatekelezwa kwa kipindi cha miaka 5 katika mikoa ya Kigoma, Tabora na Songwe na utekelezaji wake umeanza mwaka 2022.