Joy FM

Hali ya upatikanaji wa maji vijijini ni asilimia 74 Kigoma

8 November 2024, 17:53

Mkuu wa Mkoa Kigoma Kamishna Jenerali Mstaafu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye akiwa na viongozi wengene mara baada ya kukabidhigari ofisi ya Ruwasa Mkoa, Picha na Josephine Kiravu

Mkuu wa Mkoa Kigoma, Thobias Andengenye ameutaka Wakala wa Maji Mijini na Vijijini (RUWASA) Mkoa Kigoma kuhakikisha upatikanaji wa vitendea kazi kwenye sekta ya maji unajibu mipango ya Rais Samia katika kusogeza huduma karibu na wananchi ya kumtua mama ndoo kichwani.

Na Josephine Kiravu – Kigoma

Mkuu wa mkoa wa Kigoma kamishna Jenerali mstaafu wa jeshi la zimamoto na uokoaji Thobias Andengenye amekabidhi gari moja lililotolewa na Serikali kwa ajili ya uratibu wa shughuli za wakala wa maji na usafi wa mazingira vijijini (RUWASA) mkoa wa Kigoma na  kusisitiza utunzaji wa vitendea kazi vya umma kwa ajili ya kufanikisha utoaji huduma kwa wananchi.

Ni gari liliotolewa na Serikali kwa ajili ya kurahisha shughuli za RUWASA Kigoma, Picha na Josephine Kiravu

Akizungumza katika hafla fupi ya kukabidhi gari hilo, mkuu wa mkoa amesema hali ya upatikanaji wa huduma ya maji katika maeneo ya vijijini imefikia aslimia 74 ambapo kabla ya utekelezaji wa miradi ya maji inayotekelezwa hivi sasa ilikuwa ni asilimia 54.

Sauti ya Mkuu wa mkoa wa Kigoma kamishna Jenerali mstaafu wa jeshi la zimamoto na uokoaji Thobias Andengenye

Kwa upande wake, Meneja wa RUWASA mkoa wa Kigoma Mha Mathias Mwenda amesema kupatikana kwa usafiri huo kutarahisisha ufuatiliaji wa hali ya utoaji na upatikanaji wa huduma ya maji katika maeneo ya vijijini.

Sauti ya Meneja wa RUWASA mkoa wa Kigoma Mha Mathias Mwenda

Hata hivyo mhandisi Mwenda ameishukuru serikali ya awamu ya sita kwa kuboresha mazingira ya utendaji kazi katika sekta hiyo ili kuimarisha utoaji wa huduma kwa wananchi.

Mkuu wa Mkoa Kigoma Kamishna Jenerali Mstaafu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye akiwa na viongozi wengene mara baada ya kukabidhigari ofisi ya Ruwasa Mkoa, Picha na Josephine Kiravu