Joy FM

Wanavyuo watakiwa kukemea vitendo vya ukatili Kasulu

7 November 2024, 14:50

Pichani ni Mkaguzi msaidizi wa polisi ambaye pia ni Mkuu wa kitengo cha dawati la jinsia wilaya ya Kasulu Maimuna Omari wakati akizungumza na wananchuo wa FDC Kasulu.

Mkaguzi msaidizi wa Polisi ambaye pia ni Mkuu wa dawati la jinsia Wilaya Kasulu Maimuna Omary amesema ili kukabiliana na vitendo vya ukatilii ambavyo vimeendelea kutoa kwenye jamii hukuu watoto na wanawake wakiwa ndio waathirika amewataka wadau kuendelea kushirikiana kufichua vitendo hivyo.

Hagai Ruyagila – Kasulu

Wana vyuo katika vyuo mbalimbali wilayani Kasulu mkoani Kigoma wametakiwa kukemea na kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia ili kujenga jamii yenye maadili mema.

Wito huo umetolewa na Mkaguzi msaidizi wa polisi ambaye pia ni Mkuu wa kitengo cha dawati la jinsia wilaya ya Kasulu Maimuna Omari wakati akizungumza na wananchuo wa FDC Kasulu.

Afande Maimuna amesema ni jukumu la kila mwananchi kusimama kidete kukemea vitendo vya ukatili pamoja na wanachuo kukemea vitendo hivyo chuoni ili kujenga ustawi imara katika jamii.

Sauti ya Maimuna Omary

Kwa upande wake Mchungaji kiongozi wa kanisa la Kristo mfalme anglikana Murusi ambaye pia ni mkurugenzi wa kanda ya Kasulu Mjini Canon Laurent Magogwa amesema vitendo vya ukatili vinaweza kuongezeka ikiwa jamii haitakuwa na hofu ya Mungu huku akitoa wito kwa mamlaka zinazohusika kukemea vitendo hivyo.

Mchungaji kiongozi wa kanisa la Kristo mfalme anglikana Murusi ambaye pia ni mkurugenzi wa kanda ya Kasulu Mjini Canon Laurent Magogwa, Picha na Hagai Ruyagila
Sauti ya Mchungaji Magogwa

Baadhi ya wananchi wilayani Kasulu wameiambia radio joy kuwa ili kukomesha vitendo hivyo ni pamoja na maafisa ustawi wa jamii kushirikiana na viongozi wa dini kutoa elimu ya madhara ya ukatili ili kuijenga jamii yenye maadili mema.

Sauti za wananchi