Joy FM

Wazee walia na ukosefu wa dirisha la matibabu Buhigwe

7 November 2024, 10:09

Ni baadhi ya wazee wa wilaya ya Buhigwe Mkoani Kigoma wakiwa katika kikao, Picha na Mtandao

Baadhi ya wawkilishi wa Wazee Wilayani Buhigwe wameishukuru Serikali ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania kutambua kwamba wazee ni rasilimali na hazina kubwa katika maendeleo ya nchi na kuomba serikali sasa kuendelea kutatua changamoto zilizopo ikiwemo ukosefu dirisha la matibabu.

Na Michael Mpunije – Buhigwe

Baraza la wazee wa Kata ya Kinazi Wilayani Buhigwe Mkoani Kigoma wameiomba serikali Kutenga dirisha maalumu katika vituo vya kutolea huduma za afya  kwa ajili ya matibabu ya wazee pamoja na kutoa bima za afya kwa wazee ambao bado hawajapatiwa bima hizo.

Kata ya kinazi inajumla ya wazee 780 ambapo kati yao wazee 250 tayari wameshapatiwa bima za afya kulingana na taarifa ya mwenyekiti wa Baraza hilo.

Ni baadhi ya wazee wa wilaya ya Buhigwe Mkoani Kigoma wakiwa katika kikao, Picha na Mtandao

Katika taarifa hiyo kwa wananchi,viongozi wa kata na viongozi wa serikali Mwenyekiti wa baraza la wazee wakata ya kinazi Mwl mstaafu Fedes mdala ameomba baadhi ya wazee kupatiwa bima za afya pamoja na kutengwa kwa dirisha maalumu kwa ajili ya matibabu ya wazee katika zahanati ya kijiji cha kinazi.

Sauti ya Mwenyekiti wa baraza la wazee wakata ya kinazi Mwl mstaafu Fedes

Afisa maendeleo ya jamii halmashauri ya wilaya ya Buhigwe Christopher kajange amewashauri baadhi vijana wenye uwezo kiuchumi kuwawezesha wazee wao kupata bima za afya huku  akieleza kuwa atahakikisha wanatenga dirisha maalumu kwa ajili ya matibabu ya wazee.

Sauti ya Afisa maendeleo ya jamii halmashauri ya wilaya ya Buhigwe Christopher kajange

Naye mganga mfawidhi katika zahanati ya kijiji cha Kinazi Dkt Denice Yassin amesema licha ya kukosekana kwa dirisha hilo lakini wamekuwa wakitoa kipaumbele kwa wazee kupatiwa matibabu.

Sauti ya mganga mfawidhi katika zahanati ya kijiji cha Kinazi Dkt Denice Yassin