Joy FM

Nguvu ya wananchi yatumika kupata huduma za afya na shule Buhingwe

6 November 2024, 15:34

Katika picha ni Mkuu wa Wilaya Buhigwe Kanali Michael Ngayalina akiwa na wanafunzi katika moja ya shule wilayani humo, Picha na Mtandao

Serikali katika halmashari ya Wilaya ya Buhigwe Mkoani Kigoma imesema inaendelea na kujenga na kukarabati miundombinu mbalimbali ikiwemo shule ili kupunguza msongamano wa wanafunzi darasani.

Na, Michael Mpunije

Serikali wilayani Buhigwe Mkoani Kigoma imekamilisha ujenzi wa shule ya msingi Muvumu iliyopo kata ya Kinazi ili kupunguza msongamano wa wanafunzi katika shule ya msingi Kinazi.

Hayo yameelezwa na Mkuu wa wilaya ya Buhigwe Kanali Michael Ngayalina wakati akizungumza na kipindi hiki na kueleza kuwa awali shule ya msingi muvumu ilikuwa aneo la shule ya msingi kinazi na kufanya msongamano wa wanafunzi wa shule hizo kuwa mkubwa

Kanali Ngayalina amesema kwa kushirikiana na wananchi wa kijiji cha Kinazi wamefanikiwa kukamilisha ujenzi wa shule ya msingi muvumu ambayo kwa sasa inaendelea kutoa huduma kwa wanafaunzi pamoja na kuondoa msongamano wa wanafunzi na kwamba kukamilika kwa shule hiyo kumesaidia changamoto hiyo kutatuliwa.

Sauti ya Mkuu wa Wilaya Buhingwe Kanali Michael Ngayalina

Aidha katika hatua Nyingine kanali Ngayalina amesema serikali inaendelea kukamilisha ujenzi wa zahanati ya kijiji cha Kimara kata Ya Kinazi,zahanati ambayo imejengwa kwa nguvu za wananchi ili kuondoa adha ya kufuata huduma za afya umbali mrefu.

Sauti ya Mkuu wa Wilaya Buhigwe Kanali Michael Ngayalina