Wanawake watakiwa kutumia fursa zilizopo Kigoma kujikwamua kiuchumi
5 November 2024, 09:20
Wananawake Mkaoni Kigoma wametakiwa kutumia makongamamano mbalimbali ikiwemo Kigoma Ladies Gala ili kuweza kujifunza na kutambua fursa zitakazoweza kuwainua kiuchumi na taifa kwa ujumla.
Na Joha Sultan – Kigoma
Baadhi ya Wanawake Mkoani Kigoma wameshauriwa kutumia fursa mbalimbali zilizopo Mkoani Kigoma ili kujikwamua kiuchumi na kuleta maendeleo katika kajamii na taifa kwa ujumla.
Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Dkt. Rashid Mohamed Chuachua akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Kamishna Jenerali mstaafu wa Jeshi la zima moto na uokoaji Thobias Andengenye katika kongamano la wanawake wa kigoma linalofahamika kwa jina la Kigoma Ladies Gala.
Nao baadhi ya wanawake waliohudhulia kongamano hilo wameeleza namna ambavyo wamejifunza ndani ya kongamano hilo.
Kwa upande wake mwandaaji wa kongamano hilo Bi. Tumsifu Matutu ameeleza lengo la kufanya kongamano hilo na kutoa rai kwa wanawake ambao hawakuhudhulia kongamano hilo.
Kongamano hilo la Kigoma Ladies Gala lilianza mwaka 2022 ambapo kwa mwaka huu 2024 ni mara ya tatu huku kaulimbiu ikisema “tuambie mwaka 2024 umefanya nini”.