Joy FM

Makala: Uboreshaji wa barabara Kigoma ulivyoinua uchumi

29 October 2024, 11:09

Muonekano wa barabara zinazojengwa Mkaoni Kigoma na kuchochea usafirishaji na kukuza uchami kwa wananchi, Picha na Lucas Hoha

Serikali Mkoani Kigoma kupitia kwa Mkuu wa mkoa huo Kamishana Jenerali Mstaafu wa Jeshi la zimamoto na uokoaji Thobias Andengenye serikali imeendelea kuufaungua mkoa wa kigoma kwa kujenga na kuboresha miundombinu ya barabara na kurahisisha Mkoa wa kigoma kufunguka kibiashara na wananchi kusafirisha bidhaa zao ndani na njee ya Nchi

Kwa kipindi kirefu Mkoa wa Kigoma ulikuwa haujaungnishwa na mikoa mingine kwenye suala la miundombinu hususani barabara hali iliyowanyima wananchi fursa za kuwekeza kwenye biashara na sasa baada ya Seriakili kuwekeza kwenye uboreshaji wa miundombinu ikiwemo baraba za lami, baadhi ya wananchi wamesema mkoa huo kwa sasa umefunguka kibiashara kutokana na juhudi za serikali za kuboresha miundombinu mbalimbali.

Karibu kusikiliza makala fupi ya Lucas Hoha inayoangazia suala la maendeleo hasa uboreshaji wa miundombinu ya barabara Mkoani na inavyochochea uchumi kukua.