Joy FM

Ufadhili wa masomo ya ufundi wawakosha wanafunzi Kakonko

22 October 2024, 09:19

Wanafunzi wa chuo cha ufundi stadi JKT Kasanda wakionyesha miongoni mwa ujuzi walioupata wa kutengeneza mfumo wa umeme, Picha na James Jovin

Serikali wilayani Kakonko imesema itaendelea kuwapa mikopo vijana wanahitimu mafunzo ya ufundi stadi ili waweze kutumia mikopo hiyo kujiajiri kupitia shughuli mbalimbali za uzalishaji mali na kujiongezea kipato.

Na James Jovin – Kakonko

Wanafunzi waliohitimu mafunzo ya ufundi stadi katika chuo cha JKT Kasanda Vocational Training Center wilayani Kakonko mkoani Kigoma wameipongeza serikali kupitia ofisi ya waziri mkuu kwa kuwafadhili katika masomo yao na hivyo kuwasaidia kutimiza ndoto zao na kuepuka kujiingiza katika Maisha hatarishi kama ujambazi, wizi na uvutaji bangi.

Wanafunzi hao wametoa kauli hiyo wakizungumza na radio Joy mara baada ya kuhitimu mafunzo ya ufundi stadi kama vile ushonaji, ufundi magari, ufundi bomba, ufundi umeme na ususi katika mahafari ya kwanza ya chuo hicho

Wanafunzi waliohitimu mafunzo ya ufundi stadi katika chuo cha JKT Kasanda, Picha na James Jovin

Mmoja wa wanafunzi hao Maongezi Rafael pamoja na Verediana Rukasi wamesema kuwa ufadhili wa mafunzo hayo uliotolewa na serikali kupitia ofisi ya waziri mkuu maarufu kama WANAGENZI umewasaidia kwa kiasi kikubwa kutimiza ndoto zao na kujiendeleza kimaisha.

Sauti ya wanafunzi hao Maongezi Rafael pamoja na Verediana Rukasi

Kwa upande wake mkuu wa chuo cha JKT kasanda Vocational Training center Major Elieza Makobwe pamoja na makamu mkuu wa chuo bwana Rusungu Nzari wamewataka wanafunzi hao kwenda kufanya kazi za kuwaingizia kipato kutokana na fani walizosomea ili kuweza kunufaika na msaada huo uliotolewa na serikali.

Mkuu wa chuo cha JKT kasanda Vocational Training center Major Elieza Makobwe, Picha na James Jovin
Sauti ya mkuu wa chuo cha JKT kasanda Vocational Training center Major Elieza Makobwe pamoja na makamu mkuu wa chuo bwana Rusungu Nzari

Bwana Mustapha Mtungwe ambaye ni afisa maendeleo ya jamii akimwakilisha mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Kakonko kama mgeni rasimi amesema kuwa serikali iko tayari kuwasaidia vijana hao kwa kuwapa mkopo kama mitaji ya kuweza kuwasaidia kuanzisha shughuli zao hivyo kujiendeleza kiuchumi na kutimizia malengo yao.

Sauti ya Bwana Mustapha Mtungwe ambaye ni afisa maendeleo ya jamii akimwakilisha mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Kakonko

Jumla ya wanafunzi 119 waliofadhiliwa na serikali kupitia ofisi ya waziri mkuu maarufu kama WANAGENZI wamehitimu mafunzo ya ufundi stadi katika chuo cha JKT Kasanda training center ikiwa ni juhudu za serikali katika kuwaokoa vijana ambao wangeishia kwenye Maisha hatarishi na badala yake wamepatiwa mafunzo ya ufundi ili kujikwamua kimaisha na familia zao kwa ujumla