Joy FM

Kamati za utoaji mikopo ya asilimia 10 epukeni rushwa

11 October 2024, 08:43

Viongozi na wajumbe wa kamati za kata wakiwa katika kikao cha kuchakata maombi ya mikopo kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu, Picha na Lucas Hoha

Serikali wilayani kasulu imewataka viongozi na kamati zinazosimamia utoaji wa mikopo ya asilimia 10 inatolewa na halmashauri kupitia mapato ya ndani kuwa waadilifu.

Na Lucas Hoha – Kasulu

Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Kasulu Mkoani Kigoma Nurfus Aziz ameziagiza kamati za kata zinazoshughulikia utoaji wa mikopo isiyo na riba  inayotokana na asilimia 10 ya mapato ya ndani kufanya kazi kwa weledi ili kuepuka mianya ya rushwa na malalamiko kutoka kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na watu wenye ulemavu wanaokuja kuomba mikopo hiyo.

Aziz ametoa maagizo hayo wakati akifunga mafunzo yaliyolenga kuwajengea uwezo viongozi na wajumbe wa kamati za kata ambao wamepewa mamlaka ya kuchakata maombi ya mikopo kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu

Amesema lengo ya mikopo hiyo inayotokana na mapato ya ndani ya Halmashauri siyo kwenda kuiga jamii bali ni kuhakikisha wanapunguza umasikini.

Sauti ya Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Kasulu Nurfus Aziz

K wa upande wake Afisa Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri ya Mji wa Kasulu  Gabriel Zacharia amesema serikali imefanya maboresha ya sheria, kanuni na miongozo ya kutoa mikopo hiyo ikiwemo kupunguza kutoka watu 10 hadi watu 5 kwa vikundi vya wanawake na vijana wanaoomba mikopo na kutoka watu 5 hadi 2 kwa watu wenye ulemavu.

Sauti ya Afisa Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri ya Mji wa Kasulu  Gabriel Zacharia

Kwa upande baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo wakiwemo Watendaji wa Kata, wamesema kuwepo kwa kamati hizo katika mchakato wa kutoa mikopo itapunguza upendeleo na malalamiko kwani sehemu ya watu wanaounda kamati hizo wanaishi na wanachi moja kwa moja kwenye kata.

Sauti za baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo wakiwemo Watendaji wa Kata