Benki ya EXIM yaahidi kutoa huduma bora kwa wateja wake
4 October 2024, 17:21
Benki ya Exim tawi la Kigoma imesema itaendelea kuboresha na kutoa huduma bora kwa wateja wake huku ikiwataka wafanyabiashara na mashirika yaliyopo mkoani kigoma kujitokeza na kuomba mikopo inayotolewa na benki hiyo kwa lengo la kukuza biashara zao.
Na Joha Sultan – Kigoma
Katika kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja, Bank ya Exim tawi la Kigoma Tanzania imewashukuru wateja wote kwa kuwa pamoja nao na kuwaahidi kuendelea kutoa huduma stahiki kwa ukaribu ili kuweza kuleta maendeleo zaidi kwa jamii na taifa kwa ujumla.
Shukrani hizo zimetolewa na Meneja wa tawi la Exim bank Kigoma ndugu Michael Tuntufye kwenye hafla fupi ambayo iliandaliwa na bank hiyo kwaajili ya kutoa shukrani kwa wateja wake.
Aidha amesema wateja ambao wanataka kupatiwa mikopo hususani mashirika pamoja na wafanyabiashara milango ya kuwakopesha iko wazi ili kuwawezesha kukuza biashara zao.
Nao baadhi ya wateja ambao ni wanufaika wa banki ya Exim wameeleza namna ambavyo banki hiyo inavyowahudumia kwa uadilifu mkubwa bila upendeleo.