Jamii yaaswa kutowaficha watoto wenye ulemavu
4 October 2024, 13:03
Wito umetolewa kwa jamii na wadau wa maendeleo kutoa taarifa za watoto wenye ulemavu na kuwafichua ili waweze kupelekwa shule na kupata elimu kama watoto wengine kwenye jamii.
Na Sadiki Kibwana – Kigoma
Wazazi na walezi Manispaa ya Kigoma Ujiji Mkoani Kigoma wameshauriwa kuwapeleka shule watoto wenye ulemavu na kuacha kuwafisha ili kuwasadia kupata elimu na ujuzi utakao wawezesha kuinuka kiuchumi na jamii kusonga mbele kimaendeleo.
Wito huo umetolewa na Mkuu Wa wilaya ya Kigoma Dkt Rashid Mohammed Chuachua katika kilele Cha wiki ya elimu ya watu wazima Manispaa ya Kigoma Ujiji akiwakilishwa na Afisa Tarafa Kigoma Kusini Mhe. Dahaye Muchuno Anney.
Aidha Afisa Elimu kutoka UNICEF mkoa wa Kigoma Bi. Eliza Sebalua amesema wamekuwa wakiendesha kampeni mbalimbali za elimu za kuwarejesha watoto shuleni kwa kushirikiana na vijiji vyote vya mkoa wa kigoma.
Kwa upande wao, walimu wanaofundisha madarasa ya watu wazima na makundi maalum wamesema kuna changamato mbalimbali zinazowakabili baadhi ya watoto wenye ulemavu kutengwa lakini jamii imeendelea kuelimika.
Wiki ya elimu ya watu wa zimaa na makundi maalumu imeadhimishwa katika viwanja vya shule ya msingi Katubuka Manispaa ya Kigoma Ujiji, madhimisho ambayo yameenda sambamba na kauli mbiu isemayo Ujumuishi katika Elimu bila kikomo kwa Ujuzi, Ustahimilivu, amani na maendeleo.