Mwenge wa uhuru wazindua mradi wa maji wa bilioni 1.6 Kasulu
19 September 2024, 11:33
Wananchi katika hamashauri ya wilaya kasulu mkoani kigoma wametakiwa kushirikiana na serikali katika kulinda na kutunza vyanzo vya maji ikiwemo kuacha kufanya shughuli za kibinadamu karibu na vyanzo hivyo.
Na Hagai Ruyagila – Kasulu
Kiongozi wa mbio za Mwenge wa uhuru kitaifa Mwaka 2024 Godfrey Eliakim Mnzava amezindua mradi wa maji katika kata ya nyamnyusi halmashauri ya wilaya ya Kasulu wenye thamani ya shilingi Bilioni 1.6 fedha hizo zikiwa ni kutoka serikali kuu program ya malipo kwa matokea P for R.
Bw. Mnzava Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi huo amewasisitiza wananchi kutofanya shughuli yoyote ya kibinadamu katika chanzo Cha mradi huo badala yake kulinda na Kutunza vyanzo vya maji ili kuepuka changamoto ya huduma ya maji katika maeneo yao.
Diwani wa kata ya nyamnyusi Nathanaeli Ndelema ameishukuru serikali kwa namna inavyotatua changamoto ya huduma ya maji kwa jamii ambapo amesema mradi huo wameupokea na wataulinda kwa namna yoyote
Nao baadhi ya wananchi wa kata ya nyamnyusi wamesema uwepo wa mradi huo utakwenda kuwasaidia kupata huduma ya maji karibu.
Mradi huo wa maji unakwenda kuwanufaisha wakazi 7000 ndani ya kata hiyo huku matarajio yakiwa ni Kwa wakazi 10,000.