Joy FM
Joy FM
13 Aprili 2026, 08:41

Mvua ni muhimukwa maisha ya binadamu, lakini inapozidi kiwango au kunyesha kwa muda mrefu, inaweza kusababisha uharibifu mkubwa wa miundombinu hasa katika maeneo mengi ya mijini na vijijini, mvua kubwa imekuwa chanzo kikuu cha changamoto za maendeleo na miundombinu.
Na Mwandishi wetu
Serikali mkoani hapa imeanza zoezi la kukarabati mtaro wa Maji uliobomolewa na mvua kali zilizonyesha siku chache zilizopita na kusababisha athari kwenye makazi, Kata ya Kipampa na maeneo jirani katika Manispaa ya Kigoma Ujiji.
Katibu Tawala Mkoa wa Kigoma Hassan Rugwa, amesema serikali imelenga kudhibiti kabisa changamoto hiyo ili kuhakikisha wakazi katika eneo hilo wanakaa katika mazingira salama kupitia uimarishwaji wa miundombinu hiyo.

Upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Dkt. Rashid Chuachua amesema sambamba na kubomoka kwa mtaro huo, makazi na mali mbalimbali za wakazi zimeathiriwa na mvua hizo.
Baadhi ya wakazi wa kata hiyo wamesisitiza ujenzi huo kufanyika kwa kuzingatia ubora ili kuepuka kujirudia kwa changamoto hiyo.

Aidha wameishukuru serikali kwa kuguswa na tukio hilo na kuchukua hatua za haraka ili kudhibiti uwezekano wa kutokea athari zaidi iwapo mvua zitaendelea kunyesha katika maeneo hayo.
