Joy FM
Joy FM
8 April 2026, 18:09

Wafanyabiashara na wajasiriamali katika Halmashauri ya Mji wa Kasulu mkoani Kigoma wametakiwa kuhakikisha wanazingatia suala la usafi wa mazingira katika maeneo yao ili kudhibiti taka ambazo zimekuwa zikizagaa katika maeneonyao.
Na Emmanuel Kamangu
Halamshauri ya Mji wa Kasulu mkoani Kigoma imeanza kuwachukulia hatua wafanyabiashara na wajasiliamali ambao hawana vitunza taka katika maeneo yao ya kazi.
Akizungumza na Redio Joy Fm, Mkuu wa kitengo cha udhibiti wa taka ngumu Halmashauri ya Mji wa kasulu Bw. Msafiri Charles amesema wamewekeza nguvu kubwa ya kutoa elimu kwa wafanyabiashara ili kuhakikisha wanakuwa na vifaa maalumu vya kutunzia taka lakini wengi wao bado wameendelea kuwa wakaidi.
Aidha Bw. Charles amesema wafanyabiashara wamekuwa wakizalisha taka ngumu kutoka katika maduka yao huku wakizitupa bila kuzingatia utaribu jambo ambalo limekuwa likipelekea kwa kiasi kikubwa mji kuwa mchafu.
Kwa upande wao baadhi ya wafanya biashara ambao wamezungumza na redio joy wamesema miongoni mwao wapo ambao siyo waelewa wanaoishi kwa mazoea na kuwa ni vema sheria isimamiwe ili kuondokana na kero hiyo.
Hata hivyo wafanyabiashara hao wameongeza kuwa elimu iendelee kutolewa ili kuhakikisha kila mmoja anatambua umuhimu wa kuwa na kitunza taka katika maeneo yake ya biashara.