Joy FM
Joy FM
31 March 2026, 10:00

Kituo cha pamoja cha biashara kati ya Tanzania na Burundi kimetajwa kuwa chachu muhimu katika kukuza uchumi na kuimarisha mahusiano ya kibiashara kati ya nchi hizo mbili za Afrika Mashariki.
Na Tryphone Odace
Wananchi Wilayani Buhigwe Mkoani Kigoma wameiomba serikali kumsimamia mkandarasi anayejenga mradi wa kituo cha pamoja cha biashara kati ya Tanzania na Burundi kinachojengwa katika mpaka wa Mnanila Wilayani Buhigwe ili kuhakikisha unakamilika kwa wakati ili kufikia malengo ya kuchochea uchumi kwa nchi hizo.
Mradi wa kituo cha pamoja cha biashara kati ya Tanzania na Burundi, unaojengwa Mnanila Wilaya ya Buhigwe ukigharimu zaidi ya shilingi bilioni arobaini na saba ikiwa ni kituo kitakachosaidia katika masuala ya usafirishaji wa bidhaa mbalimbali na kukuza uchumi.
Ukiachilia mbali kusaidia katika kukuza pato la Serikali, mradi huo unaelezwa na wananchi katika kuinua pia uchumi wao pindi utakapokamilika huku wakiomba mkandarasi kusimamiwa ili ukamilike ndani ya wakati huku Afisa mahusiano wa mradi Grace Kassimu anasema mkandarasi amekuwa akitoa asilimia kumi ya kurudisha kwa jamii.

Mhandisi wa Mradi Galaudius Tadesa amesema sehemu kuu ya mradi itakuwa na nyumba na majengo mengine ya uhakika na miundominu mingine kama daraja linatoka upande wa Burundi, na kuunganisha majengo ya utawala lenye lurefu wa kilomita 4 ili kusaidia kuingia na kutoka katika mradi huo.
Msimaizi wa mradi huo Eradius Rafael amesema kituo cha pamoja cha biashara kitakuwa na ofisi za mamlaka zote kurahisisha utoaji wa huduma, huku Kaimu Meneja TANROADS Mkoa Kigoma Mhandisi Chora Kimata akibainisha mradi huo ni mapinduzi makubwa katika kukuza uchumi na kwamba mkandarasi anaendelea na kazi vizuri.