Joy FM

Wananchi Kasulu wasogezewa huduma ya afya karibu

21 March 2026, 12:40

Muonekano wa ujenzi w mradi wa kituo cha afya Kagerankanda Kasulu, Picha na Tryphone Odace

Takribani wananchi elfu 32 kutoka vijiji vya Kata ya Kagerankanda Halmashauri ya Wilaya Kasulu Mkoani Kigoma wanatarajia kupata huduma za afya karibu baada ya Serikali kujenga kituo cha afya katika kata hiyo ambacho kipo mbioni kuanza kutoa huduma kwa wananchi

Na Tryphone Odace

Wananchi wa Kijiji cha Kagerankanda Halmashauri ya Wilaya Kasulu Mkoani Kigoma  wamepongeza serikali kwa kujenga kituo cha afya na hali itakayosadiai kupunguza vifo na kutembea umbali mrefu kwenda  kutafuta huduma za afya katika maeneo mengine.

Muonekano wa ujenzi w mradi wa kituo cha afya Kagerankanda Kasulu, Picha na Tryphone Odace

Wakizungumza na Redio Joy Fm ilipotembelea kijiji cha Kagerankanda wananchi hao wamesema licha ya uwepo wa zahanati walilazimika kwenda kutafuta huduma za afya nje ya kata yao hali iyosababisha kutumia gharama kubwa na wakati mwingine wajawazito kujifungulia njiani kutokana na umbali mrefu.

Sauti ya Wananchi wa Kijiji cha Kagerankanda Halmashauri ya Wilaya Kasulu
Muonekano wa ndani ya kituo cha afya Kagerankanda ambao kipo katika hatua za mwisho kukamilika, Picha na Tryphone Odace

Naye Afisa Mfawidhi wa Zahanati ya Kagera nkanda ambaye pia ndiye msiamamizi wa mradi wa ujenzi wa Kituo cha afya Kagerankanda Richard Joseph Marwa amesema ujenzi wa kituo hicho utakapokamilika utasaidia kuhudumia jumla ya wananchi elfu 32 kutoka katika vijiji vya kata hiyo.

Sauti ya Afisa Mfawidhi wa Zahanati ya Kagerankanda ambaye pia ndiye msiamamizi wa mradi wa ujenzi wa Kituo cha afya Kagerankanda Richard Joseph Marwa

Akizungumzia huduma zinazotolewa kwa sasa katika zahanati Kagerankanda amesema kutokana na wingi wa wananchi wa kata hiyo zahanati hiyo ililazimika kufanya kazi usiku na mchana ili kuhakikisha wanapunguza wimbi wa wagonjwa waliokuwa wakipata hudam katika zahanati hiyo.

Sauti ya Afisa Mfawidhi wa Zahanati ya Kagerankanda ambaye pia ndiye msiamamizi wa mradi wa ujenzi wa Kituo cha afya Kagerankanda Richard Joseph Marwa
Hii ni zahanati ya Kijiji cha Kagerankanda ambayo inategemewa na wananchi wa Kata hiyo, Picha na Tryphone Odace

Diwani wa Kata ya Kagerankanda  Yohana  Mwilabule amesema  ujio wa kituo hicho kutasaidia kuongeza upatikanaji wa huduma muhimu za afya kwa wananchi ambapo ameomba serikali kuhakikisha kinakamilika kwa haraka ili waaanze kupata huduma.

Sauti ya Diwani wa Kata ya Kagerankanda  Yohana  Mwilabule
Hii ni zahanati ya Kijiji cha Kagerankanda ambayo inategemewa na wananchi wa Kata hiyo, Picha na Tryphone Odace

Kwa upande wake, Afisa mtendaji wa Kata ya Kagerankanda   Banyukwa John  Makinga ameeleza kuwa ujenzi huo ulishirikisha wananchi na kufanikiwa kuanza ujenzi  wa mradi ambao unaenda sasa kumaliza kilio cha wananchi kukosa huduma muhimu za afya.

Sauti ya Afisa mtendaji wa Kata ya Kagerankanda   Banyukwa John  Makinga