Joy FM
Joy FM
11 March 2026, 17:16

Udhibiti wa bidhaa szisizo na ubora husaidia kulinda afya na usalama wa wananchi na mara nyingi bidhaa hizo kama dawa, vipodozi na vyakula ambavyo hutengenezwa bila kufuata viwango vya ubora unaotakiwa.
Na Lucas Hoaha
Wananchi Mkoani Kigoma wameomba Shirika la viwango Tanzania (TBS) kudhibiti bidhaa ambazo hazina ubora zinazotengenezwa viwandani ili kuepuka athari zitokanazo na bidhaa hizo ikiwemo kupata kansa ya ngozi
Wakizungumza kwa nyakati tofauti wananchi hao wamesema TBS wanakila sababu ya kudhibiti bidhaa hizo kwa kufanya misako ya mara kwa mara hasa viwandani ili kubaini ubora wa bidhaa kabla ya kuwafikia watumiaji.
Awali akizungumza na waandishi wa habari, Meneja Shirika la Viwanga Tanzania TBS Kanda ya Magharibi Hamis Seleleko Simon amesema tangu kuanzishwa kwa shirika hilo kanda ya magharibi wamefutilia viwanda vikubwa na vidogo 129 na kutoa leseni kwa viwanda hivyo, huku akifafanua namna wanavyofuatilia majengo yakuhifadhia chakula.

Aidha amesema shirika hilo limekuwa likifuatilia bidhaa amabazo ni hafifu zilizopo sokoni na pindi wanapozibaini wamekuwa wakiziteketeza kwa moto ili kuondoa madhara yanayoweza kujitokeza kwa wananchi.

Shirika la viwango Tanzania TBS Kanda ya Magharibi limekuwa likifanya kazi ya kukagua bidhaa hafifu kwenye mikoa mitatu yaani Kigoma, Katavi na Tabora ikiwa ni pamoja na kuchukua hatua dhidi ya watu wanaohusika kuingiza bidhaa hizo nchini.