Joy FM

Jamii yaaswa kutofumbia macho ukatili Kakonko

9 March 2026, 09:18

Katibu tawala Mkoa wa Kigoma Hassan Rugwa mwenye sutiakiwa na baadhi ya wakuu wa wilaya za Mkoa wa Kigoma kwenye maadhimisho ya siku ya wanawake, Picha na Dotto Josephati

Kutoa taarifa za ukatili ni jukumu la kila mwanajamii kwani kutasaidia kulinda maisha ya watu, kuwapatia wahanga msaada, kuzuia ukatili kuendelea na kuhakikisha haki inatendeka.

Na Dotto Josephati

Jamii Mkoani Kigoma imetakiwa kuachana na tabia ya kufumbia macho vitendo vya ukatili pale mtu anapofanyiwa vitendo hivyo ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa dhidi ya wahusika

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Uvinza Dinnah Mathamani kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Balozi Simon Siro katika kilele cha maadhimisho ya siku wanawake ambapo kimkoa yamefanyika katika Kata ya Kasanda Wilayani Kakonko ambapo amesema endapo mtu akifanyiwa ukatili na akachelewa kutoa taarifa kwa muda mwafaka itasababisha kuwepo na ugumu katika kufanya uchunguzi na huweza kumletea madhara muhanga.

Sauti ya Mkuu wa Wilaya ya Uvinza Dinnah Mathamani
Mkuu wa Wilaya ya Uvinza Dinnah Mathamani, Picha na Dotto Josephati

Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Kanali Evance Mallasa akitoa salamu za wilaya amewataka wanawake kuchangamkia fursa zinazotolewa katika maeneo yao ili ziweze kuwasaidia kujikwamua kiuchumi katika familia zao na kuchangamkia mikopo ya asilimia kumi ya halmashauri pamoja na Ile ya asilimia saba inayotolewa na benki ya NMB.

Sauti ya Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Kanali Evance Mallasa
Baadhi ya wanawake wakiwa katika maadhimisho ya siku ya wanawake Kakonko, Picha na Dotto Josephati

Naye Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Kigoma Zaituni Buyogera amewaomba wanaume kuendelea kuwaamini wanawake na kuwapatia nafasi kwenye vitengo mbali mbali katika majukumu kwani mwanamke pia ana uwezo wa kufanya shughuli hizo kwa weledi zaidi.

Sauti ya Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Kigoma Zaituni Buyogera
Miongoni mwa wanawake waliozungumza katika maadhimisho ya siku ya wanawake, Picha na Dotto Josephati

Awali kisoma risala iliyoandaliwa na Wanawake wa Mkoa wa kigoma Bi. Salome Kitwe ameishukuru serikali Kwa kuendelea kuboresha miundombinu ambayo inawasaidia Wanawake katika shughuli zao na kuwapunguzi changamoto za kufuata huduma hizo umbali mrefu huku wakiomba serikali kuwasaidia kuwatafutia masoko ya uhakika Kwaajili ya shughuli za na kuwataka Wanawake kujitokeza kugombea nafasi mbali mbali za uongozi pale Kwani wamekua nyuma katika jambo hilo.

Sauti ya msoma risala Bi. Salome Kitwe
Baadhi ya wanawake wakiwa katika maadhimisho ya siku ya wanawake Kakonko, Picha na Dotto Josephati