Joy FM
Joy FM
6 March 2026, 16:30

Bima ya afya kwa wote ni mpango unaolenga kuhakikisha kila mwananchi anapata huduma za matibabu bila kuathiriwa na gharama za matibabu hii ni baada ya serikali kuimarisha mfumo wa bima ya afya ili kuwasaidia wananchi kupata huduma bora za afya.
Na Hagai Ruyagila
Zaidi ya Wananchi 20,000 wanaotoka katika familia zenye uhitaji maalumu Wilayani Kasulu Mkoani Kigoma wameanza kunufaika na kadi za bima ya afya zinazotolewa na serikali ambazo zitawawezesha kupata huduma za matibabu bila kulipia gharama yoyote.

Akizindua rasmi zoezi hilo katika ofisi ya Mtaa wa Nyarumanga, Kata ya Kigondo Halmashauri ya Mji Kasulu, Mkuu wa wilaya ya Kasulu Kanal Isaac Mwakisu, amesema mpango huo ni sehemu ya juhudi za serikali za kuhakikisha wananchi wote wanapata huduma bora za afya bila vikwazo vya kifedha.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa halmashauri ya Mji wa Kasulu Mh, Ayubu Ngalaba amewatoa hofu wananchi ambao bado hawajapata bima kuwa na subira kwasababu zoezi hilo bado linaendelea.

Meneja wa NHIF Mkoa wa Kigoma Gwamaka Mwakyoma amesema wamekuja kutekeleza ahadi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili kuhakikisha wananchi wanapatiwa matibabu kama Rais alivyosema.

Baadhi ya wananchi walionufaika na fursa hiyo wameishuruku serikali kwa kuwawezesha kupata Bima za afya ambazo zinaenda kurahisisha upatikanaji wa huduma bora kwa urahisi.