Joy FM
Joy FM
4 March 2026, 12:23

Kulinda vyanzo vya maji ni wajibu wa kila mtu na hivyo tunapaswa kuepuka kutupa taka hovyo, kupanda miti, na kufuata sheria za mazingira ili kuhakikisha maji yanabaki safi na salama kwa wote.
Na Emmanuel Kamangu
Wananchi wa tarafa ya heru juu katika Halmashauri ya mji wa Kasulu wameendelea kuaswa kulinda na kuthamini vyanzo vya maji kwa kupuka kufanya suguli za uzalishaji katika vyanzo hivyo.
Wito huo umetolewa na Afisa tarafa ya harujuu Bw. Sabato kwizera wakati akizungumza na Redio Joy Fm, ambapo amesema wananchi wanaendela kupewa elimu hasa kuepuka kufanya shuguli za kilimo ndani ya mita sitini kutoka katika vyanzo vya maji.
Aidha Bw. Kwizera amewataka wananchi katika tarafa hiyo kuheshimu mipaka ambayo imewekwa ikiwemo mabango ambayo yamesimikwa maeneo mengi ya vyanzo vya maji yanayowataka kutojishugulisha na shuguli za uzalishaji katika maeneo hayo hali inayoweza kupelekea kuharibu uoto wa asili ambao ni rafiki na maji.
Kwa upande wao baadhi wananchi wa tarafa ya heru juu wamesema kutokana na umuhimu wa maji wanakila sababu za kuendelea kutoa ushirikiano katika kuhakikisha vyanzo vya maji vinatunzwa.
Hata hivyo wananchi hao wameiomba serikali kuendelea kulivalia njuga swala la uhifadhi wa mazingira kwa kuwapatia elimu ya mala kwa mala jambo linatakaloweza kusaidia wengi wao kuheshimu vyanzo vya maji.
