Joy FM

Utoaji chakula shuleni Wilaya ya Uvinza umefikia 60%

2 March 2026, 09:23

Mkuu wa Wilaya Uvinza akizungumza katika kipindi cha Goodmorning Kigoma Joy Fm, Picha na Mwandishi wetu

Chakula shuleni ni nguzo muhimu katika kuhakikisha mwanafunzi anakuwa na afya njema, anafaulu masomo, na anakua katika mazingira bora ya kielimu.

Na Mwandishi wetu

Wilaya ya Uvinza imejipanga kuendelea kuboresha utoaji wa chakula shuleni ikiwa ni mkakati mojawapo wa kuongeza ufaulu kwa wanafunzi. 

Hayo yameelezwa leo Jumatatu Machi 2, 2026 na Mkuu wa Wilaya ya Uvinza Mheshimiwa Dinnah Mathamani, wakati akizungumza kupitia kipindi cha Good Morning Kigoma, kinachorushwa na Radio Joy FM.

Mkuu wa Wilaya Uvinza akizungumza katika kipindi cha Goodmorning Kigoma Joy Fm, Picha na Mwandishi wetu

Amesema kwa sasa utoaji wa chakula shuleni katika Wilaya ya Uvinza umefikia asilimia 60%, na kwamba kiwango hicho bado hakiridhishi. 

Hata hivyo Mheshimiwa Dinnah Mathamani amesema hatua hiyo inakabiliwa na changamoto ya mwitikio mdogo wa jamii kuchangia katika juhudi za serikali za kuinua kiwango cha taaluma. 

Amewahimiza wazazi wilayani Uvinza kuona umuhimu wa kuchangia chakula kwa ajili ya watoto wao shuleni na kusisitiza kuwa ni agizo la serikali kwa kila shule kwa kushirikiana na wazazi kuhakikisha wanafunzi wanapata chakula wawapo shuleni.

Mkuu wa Wilaya Uvinza akizungumza katika kipindi cha Goodmorning Kigoma Joy Fm, Picha na Mwandishi wetu