Joy FM

Wito watolewa kuchangia damu kwa wahitaji Kasulu

3 February 2026, 14:25

Sababo Kwizera ambaye amemukilisha Mkuu wa Kilaya ya Kasulu Kanal isack Mwakisu  katika hafla ya uchangiaji damu iliyoandaliwa na Jumuiya ya kiislam JAI Mkoani Kigoma, Picha na Emmanuel Kamangu

Wito umetolewa kwa wadau mbalimbali kuendelea kujitokeza kuchagngia damu ili kuweza kuokoa maisha ya wahitaji.

Na Emmanuel Kamangu

Jamii na taasisi mbali mbali za dini Wilayani Kasulu Mkoani Kigoma zimetakiwa kujenga utaratibu wa kujitolea kuchangia damu ili kusaidia hospital wilayani humo kuwa na bank ya damu salama ya  kutosha .

wito huu umetolewa na Afisa tarafa ya  heru juu  B., Sabato kwizera ambaye amemuwakilisha mkuu wa wilaya ya kasulu Kanal  Isack Mwakisu katika hafla ya uchangiaji damu ambayo imeandaliwa na jumuiya ya kiislamu Jai mkoani kigoma kwa kushirikiana na baraza kuu la waislam Tanzania wilayani kasulu zoezi ambalo limefanyika katika hospital ya mji kasulu mlimani ambapo amesema kila mwanajamii anatakiwa kuguswa na swala la kuchangia damu salama kutokana na ulihataji mkubwa ulipo.

Kwa upande wake, Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Mji Kasulu Dkt. Peter Janga amesema kujitolea kiungo cha mwili kwa ajili ya watu wengine ni upendo wa kipekee na kuwa kila mmoja anapaswa kupongeza kitendo hicho cha uungwana.

Aidha mratibu jumuiya ya kiislam JAI Mkoani Kigoma Haizuru Haruna pamoja na mwenyekiti wa Bakwata wilayani kasulu shekhe Ruheta Husein wamesema imekuwa ni utaratibu wao wa kujitolea damu salama ikiwa ni kuendelea kushirikiana na serikari kuhakikisha hospitali mbali zinakuwa akiba ya kutosha ya damu salama kwa ajili ya wahitaji.

Katika zoezi hilo jumla ya chupa 120 za Damu zimepatikana ikiwa ni hatua nzuri ya kuendelea kukabaliana na uhaba uliopo wa Damu salama katika halmashauri ya mji wa kasulu.