Joy FM
Joy FM
28 January 2026, 15:04

Familia ni msingi muhimu sana katika malezi na ukuaji wa mtoto kwani mtoto hupata upendo, ulinzi, maadili na mwelekeo wa maisha, hata hivyo, pale migogoro inapojitokeza mara kwa mara ndani ya familia, huathiri vibaya maendeleo ya ukuaji wa mtoto katika nyanja mbalimbali za maisha yake.
Na Orida Sayon
Migogoro ya ndoa kati ya baba na mama katika familia imeelezwa kuwa changamoto inayoathiri maendeleo ya ukuaji wa mtoto kijamii, kihisia, kisakolojia na kitabia.
Hayo yameelezwa na Afisa maendeleo ya jamii Manispaa ya kigoma ujiji, Eliud Galkan wakati akizungumza na Joy Fm ambapo ameeleza kuwa asilimia kubwa migogoro ya ndoa katika familia imekuwa ikisababisha matokea hasi yanayoathiri maendeleo ya makuzi ya watoto.
Kwa upande wake, Afisa ustawi wa jamii Mfawidhi Epheta Msiga amesema mila na desturi za jamii zetu zimekua chanzo cha migogoro ya ndoa kwa kuchochea ndoa katika umri mdogo.
Aidha Kaimu Afisa Dawati la jinsia na watoto Kigoma Diana Kadigi ameitaka jamii kutatua changamoto zinazotokana na migogoro ya ndoa na kudai kuwa ni chanzo cha kuondoa upendo na amani katika jamii.
Kukumbuka kuwa mtoto ni taifa la kesho anapaswa kulindwa , kupewa haki ya malezi chanya , kuheshimu haki za mtoto na kutoshirikishwa katika migogoro ya kifamilia ili kumjenga kihisia , kisaikolojia, na kijamii katika malezi na ,makuzi.