Joy FM
Joy FM
28 January 2026, 13:19

Kanisa la EAGT Jimbo la Kasulu Mkoani Kigoma limesema litaendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania kwa kuiombea ili kuhakikisha taifa linaendelea kuwa na amani, utulivu na utekelezaji bora wa miradi na mipango ya maendeleo.
Kauli hiyo imetolewa na Askofu wa Kanisa la EAGT Jimbo la Kasulu, Askofu John Kenja, wakati wa Ibada ya umoja wa makanisa ya EAGT tarafa ya Buyonga iliyofanyika katika kanisa la EAGT kwaga halmashauri ya wilaya ya Kasulu.
Askofu Kenja amesema kuwa kanisa lina wajibu wa kushirikiana na serikali kwa kutoa elimu kwa jamii, kuhimiza maadili mema, kudumisha amani na mshikamano wa kijamii, pamoja na kuwa mstari wa mbele katika kuleta maendeleo endelevu.
Mchungaji wa kanisa la EAGT Kambi ya Jeshi la Waebrania lililopo halmashauri ya Mji Kasulu, Mchungaji Abel Kasela amesema kanisa litaendelea kuhimiza umoja, amani, mishikamano na ushirikiano kati ya wananchi na seriakli kama msingi muhimu wa maendeleo.

Baadhi ya waumini wa Kanisa la EAGT Jimbo la Kasulu wamesema wako tayari kufuata maelekezo ya viongozi wao wa Kiroho, wakisisitiza kuwa kushirikiana na serikali ni jambo la msingi sana ambapo wameahidi kuendelea kuiombea serikali pamoja na viongozi wake ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi na kwa manufaa ya taifa.
