Joy FM
Joy FM
26 January 2026, 10:02

Jeshi la Polisi Nchini Burundi limefanikiwa kuzima moto ambao ulikuwa unateketeza soko la Siyoni na kusababisha taharuki kwa wafanyabiashara
Na Bukuru Daniel
Wakazi wa Bujumbura karibu na soko la Jiji, linalojulikana kama Siyoni, wanasema magari ya zima moto na polisi wa Burundi walifanikiwa kuzima moto mkubwa ulioteketeza sehemu ya soko hilo Jumapili usiku.
Watu mbalimbali kwenye mitandao ya kijamii Jumapili usiku walisambaza picha za moto mkubwa ambao umeteketeza sehemu ya soko ambapo karibu na ambako wafanyabiashara na mafundi cherehani ndilo lililolengwa na moto huo,chanzo cha moto huo kikiwa bado hakijajulikana.

Moto huo ulizuka mwendo wa saa nane usiku siku ya Jumapili na kusababisha uharibifu ambao bado haujajulikana.
Soko la Siyoni ni mojawapo ya soko kubwa zaidi mjini Bujumbura, likichukua nafasi ya soko jkuu la Bujumbura, ambalo liliharibiwa na moto mkubwa mwanzoni mwa 2013.

Wakati huo, bidhaa zenye thamani ya zaidi ya faranga bilioni 100 za Burundi ziliharibiwa na zaidi ya watu 3,000 waliokuwa wakifanya biashara katika soko hilo walipoteza mali zao, kulingana na mamlaka,soko bado halijajengwa tena hadi kufikia sasa.