Joy FM
Joy FM
20 January 2026, 15:28

Jeshi la Polisi limewasihi wafanyabiashara kuwa waaminifu na kuepuka udanganyifu katika kupima mazao ikiwa ni pamoja na kutumia serikali ya kata na mtaa kutatua kero zinazojitokeza katika eneo lao
Na Emmanuel Kamangu
Wafanyabiashara wa mazao katika soko la Mnadani Kata ya Kigondo Halmashauri ya mji wa Kasulu wamelalamikia Peshi la polisi Wilayani humo kwa kutekeleza zoezi la ukamati katika eneo hilo pasipo kufuata taratibu.
Wafanyabiashara hao wa soko la mazao munadani wakizungumza katika kikao ambacho kimeketi pamoja na mkuu wa polisi jamii wilayani kasulu ASP Masangola Kitina wamesema kumekuwa na ukamataji wa wafanyabiashara wa mazao ya nafaka bila kushirikisha uongozi wa soko hilo jambo ambalo wametaja limekuwa likileta taharuki.
ASP Kitina akijibu malalamiko hayo amewataka wafanyabiashara wa nafaka Munadani wilayani humo kuhakikisha kila mmoja anakuwa mlinzi wa mwenzake ili kukabiliana na wizi mdogo mdogo ambao umekuwa ukijitokeza eneo hilo.
Aidha ASP Kitina amewasihi sana wafanyabiashara hao kuwa waaminifu kwa kuepuka udanganyifu katika kupima mazao ya mkulima ikiwa ni pamoja na kutumia serikali ya kata na mtaa kutatua kero zinazojitokeza eneo hilo.
Hata hivyo ASP Kitina ameongeza kuwa ili kukomesha wizi mdogo mdogo katika soko la nafaka Munadani wafanyabiashara wanapswa kuwa na utu kwa kuthamini mali za jirani ili kuwa rahisi kutoa taarifa pindi wanapomuona mshukiwa wa wizi.