Joy FM

Kigoma waaswa kuchukua tahadhari majanga ya moto kwenye usafiri

16 January 2026, 14:15

Mrakibu Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoani humo ASF Michael Maganga, Picha na Sadiki Kibwana

Jeshi la Zima moto na uokoaji Mkoani Kigoma limewataka wananchi kuhakikisha wanachukua tahadhari za majanga ya moto.

Na Sadiki Kibwana

Wananchi wanaotumia bandari za Mkoa wa Kigoma wametakiwa kuchukua tahadhari mapema kabla ya kuanza kusafiri majini ili kujikinga na majanga ya moto yanaweza kujitokeza wakati wowote.

Rai hiyo imetolewa na Mrakibu Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoani humo ASF Michael Maganga wakati akitoa taarifa kwa vyombo vya habari.

Kamanda Maganga amesema kumekuwa na majanga mengi ya moto yanayotokea majini hivyo kufanyika kwa ukaguzi wa miundombinu hiyo itafanya safari ziwe salama.

Sauti ya Mrakibu Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoani humo ASF Michael Maganga

Hata hivyo, Kamanda Maganga amesema mkakati uliopo  wa kuzuia ajali za majini ni kupata boti za uokoaji ambazo ziko mbioni kuletwa mkoani hapa.

Sauti ya Mrakibu Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoani humo ASF Michael Maganga

Mkoa wa Kigoma ni mkoa ambapo umepakana na ziwa Tanganyinga na una bandari kubwa moja huku ukiwa na zaidi ya bandari ndogo 3 ambazo kwa ujumla zinafanya kazi ya kusafirisha watu na mizigo yao kila siku kuelekea maeneo mbalimbali.

Kauli hiyo ya Mrakibu Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoani Kigoma ASF Michael Maganga imekuja ikiwa ni siku moja baada ya boti kuteketea kwa moto na kusababisha majeruhi na mali zilizokuwemo kuungua