Joy FM
Joy FM
9 January 2026, 11:53

Mikopo ni nyenzo muhimu ya kuwawezesha vijana, wanawake na watu wenye ulemavu katika kujenga maisha bora na kuchangia maendeleo endelevu.
Na Orida Sayon
Baadhi ya wananchi katika Manispaa ya Kigoma Ujiji hasa vijana wameomba kuendelea kupewa elimu ya mikopo ya asilimia 10 kutoka katika mapato ya halmashauri.
Wameeleza hayo wakati wa mazungumzo na kituo hiki mazungumzo yaliyolenga kufahamu ni upi uelewa wa makundi ya wanawake, vijana, wazee na wenye ulemavu kuhusu mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na halmashauri mbalimbali hapa nchini.

Na hapa Joy Fm, inafika katika moja ya kikundi cha Womens and Children Group ili kujua wameweza je kufikia hatua ya kupata mkopo kutoka halmashauri na vijana ambao bado hawajapata mikopo kujua uelewa wao na hapa wanaeleza.
Naye Afisa maendeleo kutoka Manispaa ya Kigoma Ujiji Jabir Majira amesema serikali imeendelea kutoa mwongozo na elimu ya namna ya kupata mikopo hiyo pamoja na namna ya kutumia, kusimamia na kuendesha miradi akidai awamu ya kwanza serikali ilipata hasara kwa baadhi ya makundi kushindwa kurejesha.

Aidha Bw. Majira amesema katika mwaka wa fedha 2025/2026 Manispaa ya Kigoma Ujiji wametenga milioni 500 kwa ajili ya makundi yay a wanawake, vijana ,wazee na watu wenye ulemavu