Joy FM
Joy FM
7 January 2026, 14:21

Ujenzi wa soko la Mwanga Manispaa ya Kigoma unaoendelea unatajwa kuwa utakapokamilika utasaidia wafanyabiashara kupata sehemu salama ya kufanyia biashara zao.
Na Mwandishi wetu
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Balozi Simoni Nyakoro Sirro amemtaka Mkandarasi wa Ujenzi wa Soko la Mwanga kukamilisha ujenzi kwa wakati kutokana na kuongezewa muda wa Kazi.
Balozi Sirro ametoa agizo hilo leo Januari 7, 2026 alipofanya ziara ya kutembelea maendeleo ya ujenzi wa soko huku akisema wananchi wanasubili kuanza kutumia Soko hilo.

Amemtaka mkandarasi wa ujenzi kukamilisha ujenzi kwa wakati na kufikia mwezi mei, 2026 awe amekabidhi mradi ili uanze kuwanufaisha Wananchi.
Akitoa taarifa ya mradi, Mhandisi wa Ujenzi kutoka Kampuni ya ujenzi ya Asabhi Contractor Company Ltd in Jv with Pioneers Builders Limited Eng. Joseph Marando amesema uchelewaji wa mradi umetokana na changamoto ya mvua kubwa mwanzoni mwa utekelezaji wa mradi.

Amesema tayari wamepewa muda wa ziada wa siku 115 na wanatarajia kukamilisha ujenzi april 24 mwaka huu huku maendeleo ya ujenzi wa mradi ukiwa asilimia hamsini na moja (51.59%).
Serikali ya awamu ya sita inatekeleza ujenzi wa soko la Mwanga na Mwalo wa Katonga kwa thamani ya zaidi ya bilioni kumi na Sita (Tsh 16,495,359,710.28/=) kwa lengo la kuboresha miundombinu, kukuza uchumi wa Wanannchi na huduma kwa jamii.

Soko la Mwanga kutakuwa na maduka na vizimba, vyoo vya kawaida, vyoo vya walemavu, vibanda vya chakula, maegesho ya magari, Ofisi na Kituo cha Polisi kwa eneo la jengo lenye mita 23,872.