Joy FM

DC Buhigwe apongeza wananchi kwa juhudi za kuleta maendeleo

30 December 2025, 12:37

Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe Michael Ngayalina, Picha na Mtandao

Wananchi Wilayani Buhigwe Mkoani Kigoma wamepongezwa kwa hatua ya kuongeza juhudi za kuchochea shughuli za maendeleo zilizosaidia kukuza uchumi wa familia na Taifa kwa ujumla.

Na Josephine Kiravu

Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe Michael Ngayalina amewapongeza wananchi Wilayani humo kwa kuweka juhudi za pamoja kuleta maendeleo yenye mchango mkubwa katika kuikuza Wilaya hiyo na kuifanya kuwa ya tofauti huku akiwataka kuzidisha uwekezaji kwenye  sekta ya kilimo.

Akizungumza na wananchi hao Mkuu wa wilaya amewataka kufanya vizuri hasa kipindi hiki cha kilimo kwa kuhakikisha wanazingatia kilimo cha kisasa pamoja na kusisitiza kuwatumia maafisa ugani ili wapate mazao mengi na kuinua wilaya hiyo kiuchumi na kuendelea kuwa kivutio kwa wakazi wa maeneo mengine.

Sauti ya Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe Michael Ngayalina

Wananchi wa wilaya ya Buhigwe wanasifika kwa kilimo cha ndizi na kahawa ambapo wakazi wa maeneo jirani hutegemea soko la ndizi katika maeneo mbalimbali ya wilaya hiyo jambo ambalo linaendelea kuitangaza wilaya ya Buhigwe hasa kwenye sekta ya kilimo.

Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe Michael Ngayalina, Picha na Mtandao