Joy FM
Joy FM
29 December 2025, 15:55

Wakati mashirika ya kimataifa yakieleza kuwa Burundi ni miongoni mwa nchi masikini zaidi duniani, Rais wa nchi hiyo amesema watu wa nchi hiyo wana furaha.
Na Bukuru Daniel
Rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye anasema anaiona nchi yake kama nchi ya watu wenye furaha na kuna dalili kwamba uchumi wa raia wake unaendelea kuimarika.
Katika hotuba yake aliyoitoa katika ukumbi wa Uwanja wa Royal uliopo Muramvya katika mkoa wa Gitega, akielezea hali ya maisha nchini mwaka huu unapokaribia kuisha, Ndayishimiye aliangazia baadhi ya mambo ambayo serikali yake inajivunia.
Alisema mwaka huu Burundi iliandaa uchaguzi ambao ulikwenda vizuri na salama, bila mizozo kati ya watu, bila watu kutazamana kwa jicho baya, kwa upande wa uchumi na ustawi wa watu, Rais Ndayishimiye alisema kuwa Warundi wanaongeza mapato yao kwa njia inayoonekana.
Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) linasema pato la Taifa la Burundi lilikua kwa 4.4% mwaka huu hadi dola bilioni 7.
Wakati pato la taifa la Warundi kwa sasa ni dola 486 kwa kila mtu, kwa mujibu wa IMF, nchi zenye Pato la Taifa la chini zaidi duniani ni Afghanistan ($417), Yemen ($415) na Sudan Kusini ($313).
Ndayishimiye anasema miongoni mwa mafanikio hayo ni kuongezeka kwa upatikanaji wa umeme nchini’ ambapo tangu 2020, umeongezeka zaidi ya mara tatu .
Alipongeza kuwa sekta ya madini kwa sasa inafanya kazi vizuri huku akibainisha kuwa mwaka huu imeingiza mapato ya dola za Marekani milioni 12 na kutoa ajira kwa maelfu ya watu.