Joy FM

Jamii Kasulu yaaswa kutumia mitandao ya kijamii kwa njia chanya

29 December 2025, 09:45

Askofu wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya western Tanganyika Mhashamu Emmanuel Bwatta, Picha na Hagai Ruyagila

Katika ulimwengu wa sasa, mitandao ya kijamii imekuwa sehemu muhimu ya maisha ya kila siku watu wengi hutumia mitandao kwa mawasiliano, kupata habari na kujiburudisha, hata hivyo, matumizi ya mitandao yanaweza kuwa na faida au hasara kulingana na namna inavyotumiwa.

Na Hagai Ruyagila

Askofu wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya western Tanganyika Mhashamu Emmanuel Bwatta ametoa wito kwa jamii Wilayani Kasulu Mkoani Kigoma kuitumia mitandao ya Kijamii kwa njia chanya itakayowawezesha kujipatia kipato na kukuza maendeleo yao badala ya kuitumia vibaya kinyume na maadili ya taifa.

Askofu Bwatta Ametoa wito huo wakati akizungumza na waumini wa kanisa la Mt. Andrea Anglikana Kasulu Mjini.

Amesema mitandao inamanufaa makubwa katika jamii endapo itatumika ipasavyo, ikiwemo kutangaza biashara, elimu na fursa mbalimbali za kiuchumi.

Hata hivyo ameeleza kuwa baadhi ya wananchi wamekuwa wakiitumia mitandao hiyo vibaya kutokana na kukosa uelewa wa matumizi sahihi hali inayochangia mmomonyoko wa maadili ya kitanzania.

Sauti ya Askofu wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya western Tanganyika Mhashamu Emmanuel Bwatta
Askofu wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya western Tanganyika Mhashamu Emmanuel Bwatta, Picha na Hagai Ruyagila

Aidha Askofu Bwatta amesisitiza umuhimu wa jamii kuwakemea na kuwapinga watu wote wanaotumia mitandao ya kijamii vibaya kwa lengo la kuvuruga amani na mshikamano wa nchi, akieleza kuwa tabia hiyo inaweza kuhatarisha amani iliyopo.

Sauti ya Askofu wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya western Tanganyika Mhashamu Emmanuel Bwatta

Kwa upande wake, Makamu mwenyekiti wa halmashauri ya Mji Kasulu Mh, Canon Mley Hosea Nkayamba, amewataka wananchi wanaotumia mitandao ya kijamii vibaya kuacha mara moja tabia hiyo, akisisitiza kuwa mitandao hiyo itumike kutangaza amani, umoja na maendeleo ya jamii.

Sauti ya Makamu mwenyekiti wa halmashauri ya Mji Kasulu Mh, Canon Mley Hosea Nkayamba

Nao baadhi ya wananchi wa Wilaya ya Kasulu wamesema mitandao ya kijamii inapaswa itumiwe vizuri kwa kuzingatia maadili, sheria na misingi ya taifa.

Sauti ya baadhi ya wananchi wa wilaya ya Kasulu