Joy FM
Joy FM
24 December 2025, 09:12

Serikali imesema itaendelea kutoa mikopo kwa vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu huku ikisisitiza waliopata mkopo kuzitumia kwa manufaa na kurejesha kwa wakati
Na mwandishi wetu
Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji, imekabidhi pikipiki sita kwa vikundi viwili vya wajasiriamali ikiwa ni sehemu ya mkopo wa 10% kwa makundi ya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu.

Pikipiki hizo zimekabidhiwa kwa wajariamali hao na Katibu Tawala wa Wilaya ya Kigoma Mganwa Nzota zenye thamani ya shilingi milioni 21.5 zikiwa na bima kubwa ya kukabiliana na majanga.
Aidha Mganwa Nzota amewataka wanufaika wa mikopo hiyo kusimamia pikipiki hizo ili kuwanufaisha na kuwainua kiuchumi kwa kuwapatia madereva wenye mafunzo ya udereva na Lesseni.

Naye Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma Ujiji Lawi Kajanja amesema Halmashauri inaendelea kutenga mapato ya asilimia 10 ili kuendelea kuinua uchumi wa wananchi kupitia mikopo isiyokuwa na riba.
Vikundi vilivyonufaika na mkopo huo wa pikipiki ni Kikundi cha wanawake cha Chapa kazi kilichopo Kata ya Businde kilichopokea pikipiki tatu na kikundi cha vijana cha Kazi na maendeleo kilichopo Kata ya Mwanga Kusini kikipokea pikipiki tatu.

Utoaji wa mikopo hiyo isiyokuwa na riba Manispaa ya Kigoma Ujiji ni awamu ya pili ambapo vikundi sitini na Sita vinakuwa vimenufaika kwa zaidi ya fedha za iitanzania milioni mia iita kumi na Sita.
