Joy FM
Joy FM
23 December 2025, 11:48

Asili na jadi ni msingi wa kukuza, kuhifadhi na kuendeleza utamaduni na mila kwa kuzithamini na kuzifundisha kwa vizazi vipya na kuhakikisha jamki inabaki na utambulisho imara huku ikikua na kubadilika katika njia chanya.
Na Tryphone Odace
Wito umetolewa kwa jamii mkoani Kigoma kuendelea kuwafundisha vijana mila, utamaduni na desturi za jamii husika kama njia ya kuchochea maendeleo na utu kwa jamii.
Hayo yameelezwa na Afisa Maendeleo ya Jamii Manispaa ya Kigoma Ujiji, Aida Nzowa wakati wa ibaada ya kiasili ijulikanayo kama Elombe ambayo hufanyika mara moja kwa mwaka kwa kuwakutanisha watu kutoka maeneo mbalimbali duniani.
Amesema ibaada ya jadi na asili ambayo ipo chini ya shirika la maendeleo ya kijamii katika asili na tamaduni (SHIMKIATA) ni muhimu kuendelea kuenziwa kwani inasaidia jamii kurudi kwenye misingi ya upendo na mshikamano na kusaidia watu kutofanyiana mambo mabaya.

Katika maendeleo ya sasa ambayo yamekuwa yakibadilika kila kukicha ni muhimu kukieleza kizazi cha sasa na kesho ili kiweze kukua kikifahamu na kutambua kuwa mila, asili na utamaduni ni nguzo muhimu sana katika kubadilisha jamii kuachana na vitendo viovu.
Awali akisoma risala mbele ya mgeni rasmi, Mwakilishi wa kamati ya maandalizi ya ibada hiyo Muntu Bhabhantu amesmea lengo lao ni kujenga jamii yenye mshikamo kupitia asili na tamaduni.

Kwa upande wake, Kiongozi wa wanajadi duniani Mwami Lokoko amesema jadi ina muhimu katika kuwasaidia watu kutambua chimbuko lao na misingi ya kale.

Mwami Lokoko, amesema wataendelea kufundisha kueleza umma ili uweze kufahamu na kutambua asili na jadi yao ilivyo ili iweze kuwasaidia kuishi katika misingi ya kusaidiana na kutokengeuka na kuhadaliwa na ulimwengu wa sasa.

Baadhi ya wananchi na viongozi wa kata ya Kitongoni Manispaa ya Kigoma Ujiji, walihudhuria ibada hiyo wamesema jamii kufundishwa jadi kupitia asili na tamaduni zao inasaidia kupunguza watu kufanya matendo maovuikiwemo ukatili.


Ibaada hiyo imeenda sambamba na utoaji wa misaada kwa wasiojiweza, kufungisha ndoa mbili za kimila ikiwa chini ya kaulimbiu isemayo “Elombe ni urithi wetu, Amani yetu, Umoja wetu, Faraja kwa wenzetu kwa maendeleo endelevu.