Joy FM
Joy FM
19 December 2025, 13:03

Wahitimu na wanafunzi wa vyuo mbalimbali nchini wanaosoma fani ya uandishi wa habari, wameshauriwa kuongeza ujuzi wao katika masuala ya kidijitali, ili kuepusha matumizi mabaya ya teknolojia yanayoweza kupotosha umma.
Na Orida Sayon
Wahitimu kutoka chuo cha utangazaji Ujiji Broadcasting Academy (UBA) wametakiwa kuzingatia maadili ya uandishi wa habari katika utekelezaji wa majukumu yao kuongeza ujuzi wao katika masuala ya kidijitali, ikiwemo matumizi sahihi ya akili mnemba (AI).
Amesema hayo Mkuu wa maudhui mtandaoni kutoka kampuni ya Azam media na mjumbe wa bodi ya chuo cha UBA Hassan Mhelela amesema hayo wakati wa mahafali ya kwanza ya chuo hicho yaliyofanyika katika ukumbi wa Anglikana uliopo Mjini Kigoma.

Mhelela amesema soko la ajira linahitaji wataalamu wanaozingatia kanuni na maadili ya habari ambayo yanarahisisha ufanyaji kazi.
Mkuu wa chuo cha UBA Bi. Victoria Ndekeye anaeleza namna wanavyowandaa wanafunzi wao kuhakikisha wanazingatia kanuni na maadili ya taaluma yao hasa katika matumizi ya teknolojia.
Na baadhi ya Wahitimu wakawa na haya ya kueleze kuhusu matumizi ya akili mnemba na faida za maadili ya uandishi katika majukumu yao.
