Joy FM
Joy FM
17 December 2025, 09:01

Serikali katika Manispaa ya Kigoma Ujiji imesema inaendelea kuhakikisha inatekeleza miradi yote ambayo itasaidia kuchochea maendeleo kwa wananchi
Na Lucas Hoha
Baadhi ya wananchi wa Kata ya Kagera Manispaa ya Kigoma Ujiji wamepongeza hatua ya serikali kujenga daraja katika mto Luiche hali inayotajwa kuwasaidia kuondoka adhaa kushindwa kuvuka na kurahisisha shughuli za uchumi
Wakizungumza na Radio Joy Fm, Baadhi ya wananchi hao wamesema mto huo umekuwa ukisababisha vifo hasa kwa wanafunzi wanaosoma katika shule ya Msingi Mgumile na wakulima kushindwa kufanya kazi kutokana na mto huo.

Mratibu wa mradi huo mhandisi Eliazer Ndaisaba kutoka Ofisi ya Mkugenzi wa Manispaa Ujiji, amesema mradi huo ni miongoni mwa miradi inayotekelezwa na fedha kutoka benki ya dunia na utarajia kukamilika mapema februari 2026.
Awali akizungumzia mradi huo na miradi mingine, Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma Ujiji Kisena Mabuba amesema Serikali inatekeleza miradi ambayo imesaidia kuufungua mkoa wa Kigoma, huku akiwataka wawekeza kuja kuwekeza.