Joy FM
Joy FM
16 December 2025, 13:15

Mashindano ya ujirani mwema yaliyokuwa yanaendelea katika Wilaya ya Makamba Nchini Burundi Timu kutoka Mkoa wa Kigoma Tanzania zimetolewa kwa kipigo
Na Mwandishi wetu Burungu, Burundi
Timu za wachezaji mchanganyiko za wilaya za Kibondo na Uvinza za mkoani Kigoma nchini Tanzania zimeyaaga mashindano ya ujirani mwema yanayofanyika wilaya ya Makamba mkoa Burungu nchini ambapo timu nne za Tanzania na nne za Burundi zinashiriki mashondano hayo yanayoendeshwa kwa njia ya mtoano.
Uvinza imeyaaga mashindano hayo kwa kufungwa goli 2-0 na wenyeji wa mashindano hayo Timu ya wilaya Makamba mkoa Burungu katika mashindano yanayofanyika kwenye uwanja wa Nkurunzinza Peace Park Complex ambapo timu ya Kibondo ilitolewa na Kombaini ya Manispaa ya Kigoma Ujiji kwa kufungwa goli 1-0.

Awali timu ya Kombaini ya Wilaya Buhigwe ya Tanzania ndiyo iliyokuwa ya kwanza kuyaaga mashindano hayo baada ya kufungwa na timu ya Muyinga ya nchini Burundi baada ya kutandikwa mabao 2-1 ambapo hata hivyo na timu ya mkoa Muyinga ya nchini Burundi ilitolewa mashindano kwa kukiuka kanuni za mashindano.
Mjumbe wa kamati ya mashindano hayo Wilfred Lutera amethibitisha kuwa timu ya Muyinga ya nchini Burundi iliondolewa mashindano kwa kucheza Zaidi ya wachezaji 10 wenye umri wa Zaidi ya miaka 21 wakati kanuni inataka wachezaji wote wawe chini ya miaka 20 hivyo Buhigwe kupata nafasi ya kuendelea na mashindano.

Katika mchezo mwingine timu ya Kombaini ya Wilaya ya Nyanza ilitolewa kwenye mashindano hayo kwa kufungwa goli 2-1 na kombaini ya wilaya Ruyigi hivyo lufanya timu za Tanzania mbili na Burundi kuendelea na mashindano hayo ambapo Nusu fainali itafanyika siku ya jumatano.
