Joy FM
Joy FM
3 December 2025, 13:57

Vijana Katika Manispaa ya Kigoma Ujiji wameaswa kuacha kufanya mambo yasiofaa katika jamii na Taifa kwa ujumla.
Hayo yameelezwa na Mwenyekiti Msaidizi Mstaafu wa makanisa ya CPCT Mkoa wa Kigoma, Mchungaji Augustino Japhari Kizeba wakati wa kilele cha sherehe za vijana Kanisa la EAGT Mwasenga ambapo ameeleza vijana ni nguzo ya taifa na hawana budi kujitenga na mambo yasiyofaa bali wajikite katika kufanya kazi.
Naye Mwenyekiti wa vijana Meshark Vasco amesema kuwa ameunda mikakati kwajili ya kuinua vijana kiuchumi na kiroho ili kuondokana na hali ya kuwa tegemezi.
Nao walezi wa vijana katika kanisa hilo John Goligosha Lamsoni na Bi. Frola Yohana wamesema kuwa wazazi na walezi wanao wajibu wa kuwasaidia vijana ili waweze kufikia malengo yao.
Baadhi ya vijana waliohudhuria sherehe hiyo wameeleza namna ya sherehe hiyo inavyolata umoja na mwitikio wa kukutanika kwa pamoja ili kuwa kitu kimoja.