Joy FM
Joy FM
2 December 2025, 12:39

Manispaa ya Kigoma Ujiji kupitia kwa madiwani wamazimia kuongeza kasi ya ukusanyaji wa mapato kutoka shilingi milioni 400 hadi milioni 500 ili kusaidia kuongeza kasi ya utekelezaji wa miradi kwa wananchi
Na Lucas Hoha
Baraza la madiwani katika Manispaa ya Kigoma Ujiji, limeadhimia kuongeza ukusanyaji wa mapato kutoka milioni 400 kwa mwezi hadi milioni 500 ili kuinusu Manispaa hiyo kutoka kwenye hatari ya kuondolewa hadhi ya kuwa Manispaa kutokana na ukusanyaji mdogo wa mapato.
Akizungumza kwenye kikao cha kwanza mara baada ya kuchaguliwa kuwa Meya wa Manispaa ya Kigoma Ujiji, Mussa Maulid amesema kipaumbele cha kwanza cha uongozi wake itakuwa ni kuongeza ukusanyaji wa mapato ili kuweka urahisi wa kutekeleza miradi ya maendeleo.

Naye Mbunge wa Jimbo la Kigoma Mjini Claiton Chipando mmarufi Baba Levo amesema katika suala la ukusanyaji wa mapato atashirikiana na Uongozi wa Manispaa ili kuhakikissha wanabuni vyanzo vipya vya mapato na fedha zitakazopatikana zitumike kwenye miradi ya maendeleo na kupunguza ushuru kwa wananchi.

Awali, Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma Ujiji Kisena Mabuba pamoja na mambo mengine amesema kwa kushirikiana na madiwani anayo imani kuwa watawatumikia wananchi kwa uaminifu ili kutekeleza miradi inayogusa wananchi ikiwemo afya, maji na miundombinu ya barabara.

Kabla ya kuanza kwa baraza hilo jipya la madiwani ambao wamechaguliwa na wananchi kwenye uchaguzi wameapa kiapo vha uaminifu kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania rasmi kuanza kuwatumikia wananchi.
