Joy FM

Wananchi waaswa kuendelea kulinda amani Kigoma

2 December 2025, 09:24

Katikati ni Diwani wa Kata ya Buhanda akiwa kwenye picha na walimu wa shule ya KRI wakati wa mahafali, Picha na Prisca Kizeba

Amani ni nguzo muhimu katika maisha ya binadamu na msingi wa ustawi wa jamii yoyote ile bila amani, hakuna jambo linaloweza kufanikiwa ipasavyo na ndiyo maana jamii nyingi duniani huchukua hatua mbalimbali kuhakikisha kuwa amani inadumishwa na amani si jukumu la Serikali pekee, bali ni wajibu wa kila mwananchi.

Na Prisca Kizeba

Wananchi wa Kata ya Buhanda Manispaa ya Kigoma Ujiji Mkoani Kigoma wameaswa kuendelea kulinda amani ya nchi

Hayo yameelezwa na Diwani mteule wa kata ya Buhanda Manispaa ya kigoma Ujiji Edwad Misigaro wakati wa sherehe ya wanafunzi katika shule ya KRI ambapo amesema amani ndio msingi wa maendeleo na kuwaomba wananchi kuendelea kulinda amani na kuepuka migogoro.

Sauti ya Diwani mteule wa kata ya Buhanda Manispaa ya kigoma Ujiji Edwad Misigaro

Aidha Bw. Misigaro amewaomba wazazi, walezi na  walimu kuendelea  kushikamana katika kutoa elimu bora kwa watoto na kuahidi kurekebisha barabara inayoelekea katika shule hiyo na kuleta viti mia moja kama sehemu ya kuunga mkono juhudi za kuboresha elimu.

Sauti ya Sauti ya Diwani mteule wa kata ya Buhanda Manispaa ya kigoma Ujiji Edwad Misigaro
Wanafunzi ambao ni wahitimu wa elimu ya awali shule ya KRI Picha na Prisca Kizeba

Naye mkurugenzi wa shule Shedrack Wiliam Mgeswa amesema kuwa swala la maleziya watoto ni jukumu  la wazazi na walezi kwa kuwekeza  nguvu kubwa kwa vijana, ulinzi na maarifa kwa watoto ili kuwa na kizazi bora chenye maadili mema na maarifa ya kutosha.

Sauti ya mkurugenzi wa shule Shedrack Wiliam Mgeswa

Naye Mkuu wa shule hiyo Bi. Happy Kaje amesema kuwa katika shule yao walimu wanao jukum kubwa la kuwalinda watoto dhidi ya ukatili na kuahikisha watoto wanakuwa salama kipindi chote wanapoluwa shuleni.

Sauti ya Mkuu wa shule hiyo Bi. Happy Kaje

Baadhi ya wazazi wameelezea namna ya watoto wanavyopata elimu bora katika shule hiyo.

Sauti ya wazazi